KILIMO BORA CHA ALIZETI.


Alizeti ni mazao muhimu sana ambayo
kiukweli yana faida lukuki sana pale
ambapo mtu ataamua
kuwekeza nguvu katika kulima.zai hili.
Kwani alizeti hutumika kutengeneza mafuta
ya kupikia pamoja. Pia baada ya
kukamuliwa kwa mafuta, makapi yake
hutumika kutengeneza chakula cha mifugo
ambacho kwa neno moja huitwa
(mashudu).
Hali ya hewa na udongo.
Alizeti ni zao linalostahimili ukame pia
kwenye sehemu za mvua za wastani pia
huwezwa kulimwa kuanzia ukanda wa
pwani hadi maeneo ya mwinuko. Kwa hapa
tanzania alizeti hulimwa kwa wingi katika
mkoa wa singida.
Namna ya kuandaa shamba.
Unashauriwa kutayarisha shamba lako
mapema kwa kukatua ardhi na kulainisha
vizuri. Samadi yaweza kuchanganywa vizuri
na udongo wakati wa kuandaa shamba.
Wakati sahihi wa upandaji alizeti.
Upandaji wa alizeti hutegemea sana hali ya
hewa ya eneo husika.
Maeneo yenye mvua nyingi alizeti huanza
kupandwa mwishoni mwa mwezi Januari
mpaka katikati ya mwezi Februari.
Maeneo yenye mvua kidogo alizeti
hupandwa mwezi Desemba hadi Januari.
Kiasi cha mbegu na namna ya kupanda
alizeti.
Kiasi cha kilo 3 – 4 za mbegu zinatosha
kupanda eneo la ekari moja.Panda mbegu 3
– 4 katika kila shimo moja kwa nafasi ya
sentimita 75 kutoka mstari hadi mstari na
sentimita30 kutoka shimo hadi shimo au
sentimeta 75 kwa 40 au Sentimeta 90 kwa
30 kwa mbegu kubwa.Shimo la mbegu liwe
na kina cha sentimita 2.5 – 5.
Wiki mbili baada ya kuota, punguza miche
katika kila shimo na kubakiza

KIASI CHA MBOLEA
Mbolea zinazofaa kwa kilimo cha alizeti ni
zile za kupandia na kukuzia hasa kwenye
maeneo yasiyo na rutuba.
Wakati wa kupanda tumia nusu mfuko kwa
ekari moja ya mbolea ya kupandia na
mfuko mmoja kwa ekari moja ya mbolea
ya kukuzia kwa kuigawa mbolea hiyo mara
mbili. Nusu ya kwanza iwekwe wakati wa
kupanda na nusu ya pili iwekwe wiki mbili
baadaye. au Pandia mbolea ya TSP au
DSP, au SSP na Kuzia kwa SA baada tu ya
palizi ya Kwanza (wiki mbili hadi tatu
baada ya mimea kuota)
Wakati wa kuweka mbolea angalia
isigusane na mbegu au mche wa alizeti
kwani huunguza.

Palizi.
Alizeti hukua taratibu katika wiki chache za
mwanzo. Hivyo unashauriwa kupalilia
mapema ili kupunguza hasara. Katika
maeneo yaliyo na magugu machache, palizi
moja tu inatosha. Vile vile maeneo yenye
upepo mkali, wakati wa kupalilia inulia
matuta ili kuzuia kuanguka.

Wanyama na wadudu wanaoathiri ukuaji
wa alizeti.

1..NDEGE
Alizeti hushambuliwa sana na ndege
ambao huweza kuteketeza hadi asilimia 50
ya mazao shambani.
Kuzuia
- Usipande alizeti karibu na msitu/pori-
Vuna mapema mazao yako mara baada ya
kukomaa.- Panda alizeti kwa wingi katika
shamba moja.- watishe ndege kwa
mutumia sanamu, makopo.
Weka nyuzi zinazopatikana katika kanda za
muziki, ambazo utazifunga katika miti
miwili.ambayo wakati upepo unavuma
hupiga kelele hivyo ndege huogopa.
2..Funza wa vitumba.
Funza huyu hutoboa mbegu changa
kuanzia mara tu vitumba vya maua
vikifunguka mpaka karibu na
kukomaa kwa mbegu.
Kuzuia:
- Tumia dawa yo yote ya kuulia wadudu
inayopatikana katika maduka ya mifugo.

MAGONJWA YA ALIZETI

Alizeti hushambuliwa na magonjwa
yakiwemo madoa ya majani, kutu, kuoza
kwa mizizi, shina, kichwa na
kushambuliwa na virusi.
Kuzuia:
- Tumia kilimo cha mzunguko wa mazao-
Panda mbegu safi zilizothibitishwa na
wataalamu- Choma masalia ya msimu
uliopita- tumia madawa yanayotumika
kuulia wadudu waaribifu.
Uvunaji wa alizeti.
Unashauriwa kuvuna alizeti mara tu
inapokomaa ili kupunguza hasara ya
kushambuliwa na ndege. Alizeti iliyokomaa
kichwa hubadilika rangi toka kijani kibichi
na kuwa njano. Kata vichwa na kuvianika
juani ilivikauke vizuri.
Piga piga vichwa ili kutoa mbegu za alizeti,
kisha upepete na kuendelea kuzianika ili
zikauke vizuri.
Utafiti unaonyesha kuwa mkulima anaweza
kupata magunia kati ya 10 -12 kutoka
katika ekari moja.

Comments