Hakuna mlo wa bure, kila mlo una malipo yake,kama sio leo,basi siku nyingine.
Hivyo ndivyo ilivyo misaada yote.Kama misaada yote ni budi tuilipe na riba, basi ni vyema tuitumie kikamilifu, kwa busara na hekima
Ili hatimaye itusaidie kujikomboa katika utumwa wa ombaomba

Utumwa ambao hutulazimisha kuishi katika hali ya hofu ya kudaiwa madeni,na kudhalilishwa wakati wowote.
Mtu na jamii yake hukosa uhuru kabisa nyumbani kwake.kama ni hivyo tuache tabia ya kutaka vya bure,tule tulivyo vitokea jasho na ambavyo ni halali yetu.

Tujenge moyo wa kujiamini na kujitegemea kwani mambo mengi tunayo omba kuhisaniwa,tunaweza kuyafanya wenyewe bila msaada.
Adui yako hujifunza uwezo na udhaifu wako,kisha hutumia kikamilifu nafasi ya udhaifu wako ulionao katika mashambulizi yake.
Ndivyo walivyo wahisani.wahisani wengi wanajua udhaifu wetu wa kutojiamini,na hulka ya kutojitegemea .
Hivyo hutumia nafasi hiyo kwa njia ya misaada na zawadi kutudhalilisha,nasi hukubali kudhalilishwa.
Shida kubwa ni kuwa nasi tumekubali na kuamini kuwa sisi ni wanyonge,wakati si kweli.
Hali hii imewapa mwanya wahisani kutunyanyasa wanavyotaka .

Wakati umefika lazima tujenge moyo wa kujiamini na kujitegemea na hayo tuyafanyie kazi,tuyatekeleze kwa matendo,la sivyo hatutajitoa katika makucha ya wahisani .Kuku asipo tetea vifaranga vyake, Mwewe atavibeba vyote.
Tutetee heshima yetu na vile vizuri tulivyo navyo.

Comments
Post a Comment
+255769571079